Tanzania inajivunia na utamadumi mwingi, nchi hii ina makabila zaidi ya 120 na ingawa tunameshere baadhi kuna nyingi zingine bado.
Wamasaai na Wahindi wa Kitanzania – Jiya
Kipindi cha Jiya kimeonyesha muungano wa utamaduni ya Wamasaai na Wahindi. Urafiki Jiya na Senteu wazidi kuku na baada ya Jiya kwenda kijijini kwa Wamasaai, walimkaribisha bila mashaka.
Wazanzibari - Huba
Ndani ya kipindi cha #MMBHuba tuliona kwenye harusi ya Abby jinsi familia ya Abby ilivyowapokea familia ya Nelly Zanzibar na walivyofanya harusi ya Kizanzibari.
Waswahili wa Dar es Salaam – Kitimtim
Pili na kundi lake nzima ndani ya #MMBKitimtim wanaishi Uswazi, jijini Dar es Salaam. Mji wa Dar es Salaam unajulikana na mchanganyiko lakini pia unajulika kwa kuwa na Wazaramo wengi. Tumeona jinsi utamaduni huu wa Pwani ukiwa umeonyeshwa kwa madera na ngoma ndani ya kipindi hiki.
WaNyakyusa – Jua Kali
Kipindi Anna alivyokuwa anataka kuolewa na Diba kwa mara ya kwanza familia yake nzima ilikuja kujitambulisha nyumbani kwa Anna na walikuja wakiwa wanongea lugha yao ya nyumbani.
Fuatilia chaneli ya Maisha Magic Bongo kwa burudani bora mwezi mzima