Logo
Jua Kali
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Usaliti wa Ndani: Regina, Enzo na Davis – Jua Kali

Habari
23 Juni 2024
Professa Bill aongeza watu wapya ndani ya kampuni yake, lakini nao pia wamekuja na mpango wao.
Jua Kali

Professa Bill ameongeza watu wapya kwenye kampuni yake, lakini kila mmoja ana mpango wake maalum. Regina na timu yake wameingia kwa nguvu na moto mkali. Kazi ni kubwa, lakini Regina inaonekana amerudi na kisasi dhidi ya Thomas. Davis atafanya kazi kama mwanasheria, karibu na Anna, na amekuwa kimpa Anna muda mgumu sana. Wakati Enzo atafanya kazi kama muhasibu, karibu na Frank lakini jicho lake limekuwa limuangalia Vivian kwa ukaribu sana. Regina, akiwa sio mgeni sana, amekuja na mpango maalum na lengo lake linabakia kuwa siri kubwa.

Regina, Davis na Enzo - Jua Kali

Nani ana njama na watu wa kampuni ya Prof Bill zaidi?

Jua Kali
Davis48%
Jua Kali
Regina36%
Jua Kali
Enzo16%

Kumbuka kuangalia kipindi cha #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku ndani ya DStv chaneli 160, Maisha Magic Bongo.