channel logo dark
Jua Kali
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Nani amezidi kuchepuka? – Jua Kali

Habari
17 Septemba 2024
Kati ya Peter, Maria na Anna ni nani anayeongoza kwa udanganyifu zaidi ndani ya tamthilia ya Jua Kali?
Jua Kali

Katika kipindi maarufu cha Jua Kali kwenye Maisha Magic Bongo, udanganyifu umechukua nafasi kubwa na kufanya watazamaji kukaa kwenye viti vyao kwa hamu na ghamu. Kuna watu watatu ambao wanaongoza kusaliti waume au wake zo na kila mmoja ana njia yake ya kipekee ya kusimulia hadithi za usaliti.

Peter

Peter ni mwanaume ambaye amezama kabisa kwenye lindi la udanganyifu. Peter si tu kwamba anamvutia mke wa rafiki yake Iddy, Semeni, lakini pia amejenga uhusiano wa kimapenzi na mke mwingine wa Iddy, Sophie. Hii imekuwa ni hadithi ya kusisimua huku Peter akijaribu kujinasua kutoka kwenye mtego huu wa kimapenzi. Baada ya kuchagua wa kuw nae kati ya wake wa Iddy, aliamua kujitafutia mumama kabisa, mke wake na Prof Bill ambaye alimfumania akiwa na Sophie. Je atamchagua nani?

Anna

Tunaye pia Anna, ambaye amejikuta akivutiwa na mwenzake kazini, Davis. Mahusiano yao ya siri yanazidi kunoga huku akimficha mume wake, Diba, ukweli. Anna ameweza kuvunja mipaka ya ndoa yake kwa tamaa ya mapenzi ya siri. Hii sio mara ya kwanza kwa Anna dharau mahusiano yake na Diba. Kabla ya ndoa yao ya haraka alijikuta na Bobo wakati bado anamahusiano na Diba. Je sasa hivi Diba akigundua tena kwamba Anna anamsaliti, itakuaje?

Maria

Kama hiyo bado hayatoshi, Maria anakuja na hadithi yake ya ajabu. Akiwa amechumbiwa na Frank, Maria anatarajia mtoto wa Thomas huku Frank akiwa hana habari. Na kana kwamba hiyo haitoshi, Maria pia amekuwa akichepuka na rafiki bora wa Frank, Tony kutoka Kenya. Thomas ndio kagudua kwamba mimba ya Maria ni yak wake, je atamwambia Frank ukweli?

Endelea kufuatilia tamthilia pendwa ya #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku ndani ya Dstv chaneli 160 kugundua je, ni Peter, Anna au Maria atakae kuwa wa kwanza kugunduliwa?

[poll]