Kinata MC anajivunia kuwa msanii wa kwanza kuimba Singeli kwa Kiswahili ndani ya kipindi kinachovuma cha Divas & Hustlas ndani ya Maisha Magic Bongo.
- Singeli ilianza Tandale
Muziki wa Singeli ulianzishwa katika eneo linaloitwa Mtogole, Tandale, katika wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
- Singeli ni mchanganyiko wa mitindo mitatu ya muziki
Mtindo wa muziki huu ni muunganiko wa aina tatu za muziki. Singeli ni muziki wa ngoma pamoja na densi ambapo MC huimba juu ya muziki wa taarab unaochezwa kwa haraka.
- Singeli una asili ya Kizaramo
Wazaramo ni kabila la watu nchini Tanzania wanaotoka Dar Es Salaam na Pwani, na wengi wao wanakaa Tandale.
- Singeli ilianza na shughuli mbalimbali jijini Dar es Salaam
Muziki wa Singeli ulianza kuvuma mwanzoni mwa mwaka 2000 baada ya baadhi ya MCs kufanya shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuandaa vigodoro katika mitaa ya Manzese na Tandale, na walipenda kuwaalika wanawake kucheza.
- Mwanzilishi wa kwanza wa Singeli alikuwa Bwana Msaga Sumu
Msaga Sumu anajulikana kuwa mwanzilishi wa kwanza wa muziki wa Singeli pamoja na marafiki zake.
Je, unapenda kusikiliza Singeli? [poll]
Kwa burudani zaidi, usikose kuangalia kipindi cha #MMBDivasAndHuslas kila Alhamisi saa 1 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.