Logo
jiya, slim billboard,
channel logo dark

Jiya

160DramaPG13

Siri ya Priya na Patel - Jiya

Habari
20 Mei 2024
Je ukweli kuhusu mahusiano ya Patel na Priya yatagundulika?
Jiya

Jiya ni mojawapo ya vipindi maarufu katika Maisha Magic Bongo, na katika hadithi yake kuna siri kubwa inayohusiana na rafiki wa karibu wa Jiya, Priya.Priya, amekuwa akificha mahusiano yake Patel, baba wake Jiya, sasa hivi amejikuta katika hali ngumu baada ya Jiya kupotea.. Uhusiano kati ya Priya na Patel umekuwa siri kubwa kwa muda mrefu, hasa kwa kuwa wanaishi chini ya paa moja na wazazi wa Jiya, Patel na Arwa. Priya amekuwa akijaribu kuficha uhusiano wao kwa kila njia iwezekanavyo ili kuzuia madhara yoyote yasiyotarajiwa kwa familia ya Jiya.

Picha ya Jiya na rafiki yake wa karibu Priya

Kujikita katika uhusiano wa siri huku Jiya akiwa hajulikani aliko kumeongeza shinikizo kubwa kwa Priya. Anajikuta akilazimika kuwa mwangalifu sana na vitendo vyake, akihakikisha kwamba hakuna mtu anayeshuku chochote kuhusu uhusiano wao. Hali hii imemfanya Priya awe na wasiwasi mkubwa na kuchanganyikiwa, kwani anajua hatari ya siri hiyo kufichuliwa.

Priya akiambia familia ya Jiya kwamba amepatikana

Hata hivyo, hali hii imesababisha mgawanyiko mkubwa katika moyo wa Priya. Kujaribu kuendeleza uhusiano na baba wa rafiki yake wakati huo huo akijua kuwa Jiya yupo hatarini inamfanya awe na mzozo wa ndani. Hata hivyo, anabaki kuwa na matumaini kwamba hali itarekebishwa na Jiya atarejea salama nyumbani, akimaliza mateso yake na siri zote zitafichuliwa. Kati ya Priya na Patel ni nani ana makosa zaidi kwa haya mahusiano? Tuambie hapo chini 👇

Priya na Patel - Jiya

Nani anamakosa zidi ndani ya haya mahusiano?

Jiya
Priya39%
Jiya
Patel61%

Usikose kujiunganisha na #MyDStv App kufuatilia Jiya kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 Usiku. Jiunge na maongezi yeti kwa kupitia kurasa zeru za jamii, Facebook, Twitter (X), TikTok, Instagram na YouTube.