channel logo dark
jiya, slim billboard,
channel logo dark

Jiya

160DramaPG13

Mimi Mars arejea ndani ya Maisha Magic Bongo – Jiya

Habari
29 Agosti 2024
Mimi Mars arudi kwa uzito kama Nashipai ndani ya tamthilia ya #MMBJiya
jiya

Mwanamuziki na mwigizaji maarufu, Mimi Mars, anarejea ndani ya Maisha Magic Bongo. Baada ya kufanya kazi nzuri kama Maria kwenye kipindi cha "Jua Kali." Katika hatua mpya ya kazi yake ya uigizaji, Mimi Mars sasa atacheza kama Nashipai katika kipindi kipya cha "Jiya."

Nashipai ni daktari mwenye vipaji na rafiki wa karibu wa dada yake Senteu, mhusika mwingine muhimu katika kipindi hicho. Nashipai anajulikana kwa kuwa na moyo wa huruma na kujitolea kusaidia wagonjwa wake, lakini pia anakutana na changamoto nyingi katika kazi na maisha yake ya kibinafsi.

Ujio wa Mimi Mars kwenye "Jiya" unatarajiwa kuleta msisimko na kuongeza ladha mpya katika hadithi ya kipindi hicho, kwa kuwa ameonyesha uwezo mkubwa wa kuigiza katika majukumu yake ya awali. Mashabiki wake wanatarajia kuona jinsi atakavyoumiliki uhusika wa Nashipai na jinsi uhusiano wake na wahusika wengine utavyoendelea katika msimu huu mpya.

Kwa kurejea kwenye Maisha Magic Bongo, Mimi Mars anaendelea kuthibitisha kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wachache wanaoweza kung'ara katika nyanja tofauti za sanaa na burudani.

Angalia kipindi cha #MMBJiya tangu mwanzo ndani ya tovuti yetu hapa na pia usikose kipindi cha #MMBJiya kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:3o usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.