Logo
Huba
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Happy na Juliana: Je unaweza kamuoa mtu kwa pesa zake tuu?

Habari
20 Juni 2024
Happy apambana na uke wenza ndani ya ndoa yake na JB wakati Juliana aachwa na Mzee Andrew baada ya kufumwa na Danny.
Article

Baada ya kuolewa na Chidi, Happy aliachana naye kutokana na kutoelewana. Baadaye, alipokutana na Nicole, aliolewa na JB. Ingawa JB anamzidi umri sana, aliona ni bora kuwa naye kuliko kuwa peke yake na bila pesa. Ndoa yake na JB imekuwa ngumu kutokana na JB kuwa na mke wa pili, Tima. Tima amekuwa akikwaruzana na Happy na hapendi amani nyumbani. Je, Happy atachoka na ugomvi huu au ni bora kuvumilia ndani ya ndoa hii kwa ajili ya pesa hizo?

Mzee Andrew alimpenda Juliana baada ya kumuona mjini. Juliana alikuwa akiishi maisha magumu sana, na baada ya kumpenda, Mzee Andrew alimtoa uswahilini kwao na kumleta aishi naye nyumbani kama mama wa nyumba. Moyoni, Juliana hakumpenda Mzee Andrew na maisha pale nyumbani yalikuwa magumu na Naomi pamoja na Adrian. Alijikuta akimuwaza Danny, mwanaume aliyempenda kwa dhati. Baada ya Mzee Andrew kugundua hili, aliamua kumtimua kutoka nyumbani kwake.

Fuatilia tamthilia ya #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku na tamthilia ya #MMBNuru kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku ndani ya DStv chaneli 160 pekee!

Happy au Juliana?

Pesa imempendeza nani zaidi?

Huba
Happy20%
Nuru
Juliana80%