channel logo dark
channel logo dark

Sinia

160Tamthilia16

Tamthilia ya Sinia

Habari
19 Juni 2021
Maisha yanayotegemeana yanawafanya watu wenye matabaka tofauti ya kimaisha wasiotamani kuingiliana kimaisha kujikuta wanalazimika kuwa na muingiliano wasioupenda kutokana na mahusiano, kazi na pesa unaoleta migongano mingi isiyoisha.
Sinia Twitter Cover 1500x500 V2 GENERIC

Ni tamthilia inayohusu muingiliano wenye visa vingi vinavyozaa visasi na malumbano makubwa kati ya pande mbili za watu wa maisha ya juu,ya kati na ya chini.Chanzo kikuu cha migongano kinazalishwa na familia ya kitajiri ya Mr. Venus ambaye ni mfanyabiashara tajiri pamoja na mke wake Rose ambaye ni mwanamama mwenye mafanikio makubwa katika fani ya mitindo.Kisa kikubwa kinaanza baada ya Juan ambaye ni ndugu wa damu wa Rose na mshirika wake wa kibiashara katika kampuni yao ya mitindo ambaye ni kijana anayependa starehe kupindukia na mtumiaji wa madawa ya kulevya anaathiriwa vibaya na madawa ya kulevya mpaka kufikia hatua ya Rose kuamua kumsafirisha kupelekwa rehalb nchi za nje.Mr. Venus anapata nafasi ya kumfahamu msichana mrembo Leila(stripper wa Casino) ambaye ni mpenzi wa Juan.Pengo la Juan kutokuwepo nchini linapelekea Mr.Venus kuingia kwenye mahusiano ya siri ya kimapenzi na Leila.Leila anaingia kwenye tamaa ya kuwa sehemu ya utajiri wa Mr. Venus hivyo anamshawishi Mr.Venus ampe talaka Rose na kumuoa yeye. Mr.Venus anakuwa mgumu kutoa talaka kwa Rose akihofia mgawanyo mkubwa wa mali zake.Leila anapata ushauri wa kumuua Rose kutoka kwa Marcus ambaye ni mpenzi mwingine wa Leila.Leila na Marcus wanaanza mipango ya kutaka kumuua Rose,wakilenga kwamba baada ya kifo cha Rose Leila akiolewa na Mr.Venus basi atahakikisha anamuua Mr.Venus ili abaki na utajiri atakaoufaidi na Marcus.

Cosmas na Phina ni wanandoa,Cosmas ni mfanyakazi katika kampuni ya Mr.Venus anaiba kiasi kikubwa cha pesa katika kampuni ya Mr.Venus kwa ajili ya kulipia matibabu ya mke wake Phina aliyeugua ugonjwa wa moyo.Phina ni mtaalamu mzuri wa ubunifu wa mavazi ila alikuwa akikosa umahiri wa kazi kutokana na kuugua hivyo baada ya kupona anasaidiwa na Cosmas kupata kazi katika kampuni ya Rose akichukua nafasi ya Tresha mwanamke aliyeamua kuacha kazi baada ya kudhalilishwa kingono na Juan.Mambo yanaenda vibaya kwa upande wa Cosmas baada ya wizi alioufanya kugunduliwa na Mr.Venus hivyo anafukuzwa kazi na kufunguliwa mashtaka.Cosmas anasaidiwa kisheria na mdogo wake aitwaye Adili mhitimu wa masomo ya sheria anayetafuta ajira bila mafanikio. Cosmas analipishwa faini kubwa inayompelekea kuuza magari yake na nyumba ili kulipa faini na kuepuka kifungo.Anahaha kupata ajira kutokana na CV yake kuchafuka.Phina anabeba mzigo wa kulea familia ambayo ina wanaume wawili wasiokuwa na kazi Cosmas na Adili hivyo anamshauri Adili aingie kwenye fani ya mitindo ambayo anaamini angeiweza kutokana na muonekano wake.Adili anapata wakati mgumu kuikubali fani ya mitindo baada ya kupata pingamizi kubwa kutoka kwa mpenzi wake Isabela ambao wote wamesomea sheria na wanahaha kutafuta ajira bila mafanikio.Ndoa ya Phina na Cosmas inaanza kuwa na misukosuko sana baada ya Phina kuona kwamba anasimamia kila hitaji la familia pia ujio wa Juan ambaye anarudi kutoka rehalb akiwa mzima wa afya anamtongoza Phina kwa njia zenye ushawishi mkubwa unaopelekea Phina kuazna kumdaharau mume wake,Cosmas anampata msongo mkali sana wa mawazo unaomfanya kuishi maisha ya kutokujijali yanayowashangaza wengi wanaomfahamu.Mahusiano ya Adili na Isabela yanaingia kwenye misukosuko baada ya Adili kuamua kuingia katika fani ya mitindo,Adili anavurugwa kiakili na Isabela na kujikuta akimbaka Maria msaidizi wa kazi za ndani kwa Cosmas,jambo hili linapogunduliwa na Phina Adili anatoroka nyumbani kwa kaka yake.

Mzee Kambinu ni mzee wa makamo aliyefungwa gerezani.Msamaha wa Rais unatolewa kwa baadhi ya wafungwa hasa wale waliobakiza muda mfupi gerezani.Mzee Kambinu anatoka gerezani na kurudi uraiani anapokelewa mwanaye Isabella pamoja na mkewe Bi.Lucy ambaye ni mama lishe wa uswahilini.Akiwa uraiani anaanza kumtafuta mtu anayeitwa Donald Kado bila mafanikio,anaonesha picha ya ujana ambayo alikuwa amepiga akiwa na Donald Kado ila hakuna mtu anayemfahamu pia inatokana na uchakavu wa picha ile na kuifanya kutokumuonesha vizuri Donald Kado.Baadaye inagundulika kuwa Donald Kado ni Mr.Venus huyu ni mtu aliyekuwa rafiki wa karibu sana wa Mzee kambinu,walifanya dili kubwa sana la pesa bandarini wakiwa watatu Mzee kambinu,Donald Kado(Mr.Venus) na Richard Dovu.Baada ya kupata pesa hizo Donald Kado akaamua kuwageuka wenzake na kuwabambikia madawa ya kulevya kisha kuwataarifu polisi baada ya Mzee Kambinu na Richard Dovu kukamatwa Donald Kado akabaki akiwa ameshikilia pesa zote walizopata na huo ukawa mwanza wa utajiri wa Donald Kado ambaye aliamua kubadili jina na kujiita Mr.Venus ili kujipa usalama zaidi.Baada ya Mzee kambinu na Richard Dovu kuhukumiwa,Richard Dovu alifia gerezani na Mzee Kambinu alipotoka aliapa kumtafuta Donald Kado(Mr.Venus) popote alipo achague kati ya kumpa mgao wake au kulipa kisasi.

Usikose kuangalia kipindi cha #MMBSinia kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.