Tamthilia zetu Huba, Pazia, Kitimtim na Jua Kali, harakati za mahusiano zina mambo mengi na. Tumekuwekea orodha hapo chini kumsaidia kila mtu kufanya maamuzi sahihi!
Roy (Huba)
Roy tunamjua kama mume wa Doris lakini hapo kati alihamishia majeshi kwa mrembo Nandi na hivi sasa Roy huyu huyu amekita jicho lake kwa bibie Fei na cha kushangaza zaidi Tesa nae amehamia kwa Roy. Tumsaidie kuchagua, abaki na nani?
Henry (Pazia)
Ingawa Henry anaishi na Lolita, huku nyuma ana mahusiano na Gloria. Na bado kuna Eliza na Miriam pia. Hapa anapendezana na nani?
Pili (Kitimtim)
Nani amesema kwamba ni wanaume tu ndio wanaweza kuwa na wenza zaidi ya mmoja? Bi Pili amebadilisha mchezo , huku Zunde na kula Sabufa , kazi kwako mtazamaji je ni nani amfanye baba Watoto?
Prof Bill (Jua Kali)
Uzee mwisho chainze! Professa Bill , mwamba mwenyewe ametushushia masuprise ya kutosha hivi karibuni , ni baada ya kugundulika kwamba , Aunty Zai nae ni mke halali na wana Watoto , je huu mtanange ataushinda nani na je wakubaliane kuishi kama wake wenza au mmoja atoke kumpisha mwenzake? So tuchague nani abaki mjengoni?
JB (Huba)
Majini ya JB hayajawahi kumuacha salama kabisa, licha ya kupitishwa mengi. Je Jb abaki na mapenzi mapya na Tima au arudi kwa Happy?
Iddy (Jua Kali)
Baada ya kutimiza ahadi zake na kuoa mke wa pili Sophia , nyumba imewaka moto , ni vuta ni kuvute na mke mkubwa Semeni , Je mwenye mapenzi ya dhati na Iddy hapa ni Semeni au Sophia?
Kumbuka kujiunga na #MyDStv App kuendelea kuburudika na vipindi vya #MaishaMagicBongo popote ulipo kila siku.