Sio kila mtu ana bahati ya kupata bosi mzuri, baadhi ya mabosi ndani ya vipindi vya Maisha Magic Bongo ni wakali na wajulikana kwa tabia zao mbaya. Hii ni orodha ya mabosi wanaochuwa ndani ya vipindi vyetu:
Gota – Pazia
Gota alianza kuchukiwa na fanya kazi wake baada ya kuonyesha upendekezo kwa Chamsia. Baada ya kumpandisha Chamsia cheo na mshara alianza mahusiano naye na mahusiano yao yalizidi kuchangia kuonyesha upendeleo kwa Chamsia.
Kibibi – Huba
Kibibi anajulikana kuwa mkatili sana na kama hamna utofauti. Amekuwa akimtesa Monica na mahusiano yake na Fabrizio hayaeleweki kwa watu wengi na ingawa anamuheshimu Fabrizio kuliko wafanya kazi wake wengine wote, bado kuna matatizo kati yao.
Professa Bill – Jua Kali
Bill ndiye mkuu nyumbani, na baada ya familia yake kugundua kwamba miaka iliyopita aliwahi kuwa na mahusiano na Zai, mfanyakazi wa nyumba, Bill aliamua kumuacha Zai afanye kazi kwake wakati mke wake anamchukia.
Endelea kufuatilia vipindi halisi vya kitanzania ndani ya DStv chaneli 160, Maisha Magic Bongo